Mapema mahakama ya rufaa ilikataa ombi la serikali ya Marekani la kurejesha amri ya marufuku ya kuwazuia wahamiaji ambapo ofisi ya mwanasheria mkuu imepewa hadi leo Jumatatu kujibu maamuzi hayo.
Amesema kuwa mahakama ambayo imezuia hatua hiyo inafanya kuwa vigumu kuimarisha usalama katika mipaka ya Marekani na kumshtumu jaji aliyetoa uamuzi huo kwamba analiweka taifa hilo mashakani.
Amesema kuwa iwapo kutakuwa na tukio lolote jaji huyo na mfumo wote wa mahakama utalaumiwa.
Awali mahakama ya kijimbo ilikataa ombi la serikali la kuhalalisha marufuku hiyo.
Idara ya haki ina hadi Jumatatu mchana kujibu.
chanzo:bbc.
Comments