Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakati akitoa
ufafanuzi kuhusu uvutaji wa sigara hadharani katika sehemu za mkusanyiko
na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Alisema tayari Wizara ya Afya imewasilisha muswada wa kulinda afya ya
jamii ambao moja ya kazi yake kubwa
ni kupambana na matumizi ya sigara
katika jamii na sehemu za mkusanyiko.
Akifafanua zaidi, alisema utafiti uliofanywa kuhusu maradhi
yasiyoambukiza unaonesha kwamba upo kwa asilimia 38 ambayo yanahusishwa
na uvutaji wa sigara.
Kombo alisema mwongozo huo ukikamilika utaletwa mbele ya wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi na wajumbe kutoa maoni yao kabla ya kufanya kazi
na kuwa sheria inayotakiwa kutekelezwa na kusimamiwa.
Alisema yapo matumizi mabaya ya uvutaji wa sigara hadharani ikiwemo
sehemu za mikusanyiko ya watu kama hospitalini na sehemu za kusubiri
usafiri wa abiria na kusababisha madhara makubwa ambayo hayaonekani kwa
mara moja.
chanzo:Habarileo
Comments