RC:Tajeni wanaojihusisha na ‘unga’.

MKUU wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe, amewataka wananchi wa mkoa huo kushirikina na Serikali kwa kutoa taarifa za watu wanaohusika na biashara ya dawa za kulevya kwa kufanya usambazaji, usafirishaji na ununuzi wa dawa hizo, ili vyombo vya dola viweze kuwakamata na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.

Dk Kebwe alisema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa huo (RCC) kilichofanyika jana mkoani humu.


Alisema mkoa wa Morogoro unaungana na Rais kupambana na vita hiyo na utahakikisha unapambana na wale wote wanaohusika na uzambazaji, usafirishahi, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya.

Alivitaka vyombo vya dola vya mkoa huo kufuatilia kilimo cha bangi katika maeneo ya baadhi ya wilaya za mkoa huo na kuhakikisha wale wote wanaojihusisha wanakamatwa na kupelekwa katika vyombo vya sheria.

Mkuu huyo wa mkoa aliwaagiza wakuu wa wilaya kupitia kamati zao za ulinzi na usalama kuelekeza nguvu zao kwa kuendesha misako ngazi ya vijiji na vitongoji kupitia viongozi wa maeneo hayo ili kuwabaini watumiaji, wasafirishaji na wauzaji wa dawa za kulevya ikiwemo kubaini mashamba ya bangi.

Dk. Kebwe alisema msako huo unapaswa uwe endelevu na wale watakaopatikana na makosa hayo wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani .

chanzo:Habarileo.

Comments