Nyangumi hao ni sehemu ya nyangumi 400 waliokwama baharini usiku wa kuamkia leo.
Takriban nyangumi 300 walifariki usiku katika ufuo wa Farewell Spit, katika kisiwa cha Kusini, katika kisa
ambacho kinatajwa kuwa kibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Mamia ya raia wa kujitolea wakisaidiana na maafisa wa uhifadhi wa wanyama na mazingira wanafanya juhudi za kusaidia kuwarejesha nyangumi hao baharini.
Wamekusanyika kwenye foleni kubwa kujaribu kuwaokoa nyangumi hao.
Lakini wakati mwingine inadhaniwa huwa inatokea kwa sababu nyangumi ni wazee sana au wanaugua, au wameumia, au wamepoteza mwelekeo hasa maeneo ambayo ufuo si laini.
Wakati mwingine, nyangumi anapokwama baharini, atawalilia wenzake ambao watafika kujaribu kumuokoa. Wengi mara nyingi nao hukwama maji yanapokupwa.
Idara ya uhifadhi baharini imesema ilipokea taarifa kwamba huenda kuna nyangumi waliokuwa wamekwama Alhamisi usiku.
chanzo:bbc.
Comments