Mwishoni mwa wiki maduka 30 yanayomilikiwa na raia wa kigeni yaliporwa na kuchomwa mjini Pretoria.
Lakini
msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni Clayson Monyela,
aliliambia gazeti la New Age la Afrika Kusini kuwa visa hivyo ni
vichache.
Mapema wiki hii mshauri wa rais wa Nigeria alisema watu 116 raia
wa Nigeria, wameuawa nchini Afrika Kusini katika kipindi cha miaka
mwili.
Wakati huo huo mashirika ya usalama nchini Afrika kusini
yamelaani taarifa kwenye mitandao ya kijamii baada ya mashambulizi ya
hivi majuzi kwenye mali inayomilikiwa na raia wa kigeni kwenye miji ya
Johannesburg na Tshwane.
Serikali inasema imewahakikishia watu wa nchini humo wakiwemo raia wa
kigeni kuwa mashirika ya usalama yanaelewa vitisho vinavyosambazawa
kwenye mitandao ya kijamii.
Pia wanadai kuwa wanapoteza ajira kwa raia wa kigeni.
chanzo:Bbc.
Comments