Bw Mugabe, ambaye ndiye mara ya
kwanza anazungumzia utawala wa Bw Trump, amesema alishangazwa na ushindi
wa kiongozi huyo wa Republican.
Hata hivyo, amesema hakutaka pia
"Madam Clinton ashinde", akirejelea mgombea wa chama cha Democratic
aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton.
"Lakini
vilevile, ukija kwa Donald Trump ambapo anazungumzia uzalendo...
Marekani iwe ya Wamarekani - katika hilo, nakubaliana naye.
Zimbabwe iwe
ya Wazimbabwe," Bw Mugabe amesema, kwenye dondoo ambazo zimechapishwa
katika gazeti rasmi la serikali la Herald.
Ameongeza kwamba Bw Trump anafaa kupewa muda wa kudhihirisha uwezo wake.
"Sijui. Mpeni muda. Bw Trump huenda hata labda ataangalia upya vikwazo vilivyowekewa Zimbabwe," Bw Mugabe amesema.
Mahojiano
kamili ya Bw Mugabe yanatarajiwa kupeperushwa rasmi kesho jioni kwenda
sambamba na maadhimisho ya kusherehekea kiongozi huyo kutimiza miaka 93
tangu kuzaliwa kwake.
Bw Mugabe pia amesema anafaa kuendelea kuongoza, kwani watu wengi
nchini mwake wanahisi kwamba hakuna mtu anayetosha kuchukua pahala pake.
Kiongozi huyo tayari ameteuliwa na chama tawala cha Zanu-PF kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
chanzo:Bbc.
Comments