Akizungumza katika Jukwaa la Biashara lililoandaliwa na kampuni ya
magazeti ya Serikali (TSN), Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni,
alimpongeza Mtaka akisema anashukuru mkoa huo kupata mkuu wa mkoa mwenye
uwezo kama yeye.
“Ndugu zangu, Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake
mpeni. Mkuu wetu wa mkoa anafanya mambo mazuri na makubwa sana kwa faida
ya mkoa wetu.”
Baada ya kusema hayo, Chegeni aliyekuwa ameketi meza kuu akamgeukia Mtaka.
“Ndugu mkuu wa mkoa, hakika wewe ni twiga wetu. Unaona mbali kwa ajili ya mkoa wetu.”
Akiteta na HabariLeo nje ya ukumbi kulikokuwa kunafanyika Jukwaa
hilo, Mbunge wa Itilima ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara mkoani humo, Njalu Silanga, alisema wanashukuru kuwa na
mkuu wa mkoa anayeona fursa nyingi katika mkoa huo na kutaka kuona
zinawanufaisha wana Simiyu na kwamba wana imani kuwa atasaidia sana
kuupaisha
chanzo:Habarileo.
Comments