Bohari ya Dawa
(MSD) imetia saini hati ya makubaliano ya umilikishwaji ardhi iliyopo
Misugusugu Kibaha lenye ukubwa wa kilomita za mraba 400,000 ambazo ni sawa na
ukubwa wa hekari 100.
Eneo hilo ni
maalum kwa ajili ya kuanzisha kiwanda cha dawa ili kutekeleza mradi wa
uzalishaji dawa kwa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi.
Mkurugenzi wa
MSD, Lauren Bwanakunu amesema leo (Jumatatu) kuwa eneo hilo limenunuliwa kwa
Sh2 bilioni.
chanzo:mwananchi.
Comments