Uteuzi
huo mpya ni kufuatia kufutwa kazi kwa Luteni Generali Lt Gen Michael
Flynn ambaye alihudumu katika cheo hicho kwa wiki tatu tu.
Mteule
wa sasa wa Rais Trump yaani Luteni Generali McMaster alifanya kazi
nchini Iraq na Afghanistan alikokuwa katika kitengo cha kukabiliana na
rushwa.
Rais Trump amempongeza McMaster kukubaliana na uteuzi huo
na kumuelezea kuwa ni mtu mwenye uzoefu mkubwa na anayeheshimika na kila
mmoja.
Katika kitabu chake McMaster aliwahi kulalamikia uamuzi wa majeshi ya Marekani kuhusika na vita vya Vietnam.
Ni msomi wa masuala ya historia ya Marekani kutoka chuo kikuu cha North Carolina.
chanzo:Bbc.
Comments