Takiban watu milioni 5.5 nchini Sudan Kusini wanakumbwa na hatari ya hali mbaya ya njaa.
"Haya
ni matokeo ya moja kwa moja ambayo yamesababishwa na mzozo wa muda
mrefu kutoka kwa vingozi wa Sudan Kusini, ambao hawataki kuweka kando
maslahi yao ya kisiasa kwa manufaa wa watu wao." Msemaji wa wizara ya
mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani amesema.
Kwa upande wake kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis, ametaka
msaada kutumwa kwa mamilioni ya watu wanaokumbwa na njaa Sudan Kusini.
Akiongea
mjini Vatican Papa Francis alisema kuwa ni wakati wa kujitolea zaidi,
sio kwa kuongea tu bali kwa kutoa chakula na kukiruhusu kuwafikia watu
wanaotaabika.
Sudan Kusini imekumbwa na vita tangu mwaka 2013, ambapo zaidi ya watu milioni 3 wamelazimika kukimbia makwao.
chanzo:Bbc.
Comments