Tukio hilo la kukamata dawa hizo limetokea katika kijiji cha Mzeri,
kata ya Misima ambapo Gondwe alibainisha kuwa wilaya hiyo ina matumizi
makubwa ya mirungi na bangi.
Imeelezwa kuwa dawa hizo zilikua zikisafirishwa kutoka Korogwe na
kwamba mtuhumiwa alifanikiwa kuwatoroka polisi na jitihada za kumtafuta
ili kumfikisha kwenye vyombo vya sheria zinaendelea.
“Vijana wetu wa upelelezi wamegundua utumiaji wa dawa hizo na
tutahakikisha tunawafikisha kwenye vyombo vya sheria wauzaji na
watumiaji wa dawa hizo,” alisema.
Aliongeza kuwa polisi inashirikiana na zimamoto na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kudhibiti kabisa biashara hiyo.
“Tumeunda timu ambayo mwenyekiti wake ni OCD itakayokuwa inafanya
doria usiku na mchana ili kuhakikisha vijana wetu wanabaki salama na
kukomesha kabisa biashara ya dawa za kulevya,” alisema.
Mkuu huyo wa wilaya alitoa wito kwa watumiaji na wauzaji wa dawa hizo
kuacha mara moja badala yake wajikite kwenye shughuli nyingine halali
zitakazoweza kuwainua kiuchumi.
“Jeshi la polisi halitaacha kuwafuatilia na kuwafikisha kwenye vyombo
vya sheria kwani Serikali wilayani Handeni haitakuwa tayari kuona nguvu
kazi ya vijana inateketea,” alisema.
Baadhi ya vijana wilayani humo wameunga mkono juhudi zinazofanywa na
Serikali katika kupambana na dawa za kulevya na wamesema kuwa nguvu kazi
ya vijana wengi imekuwa ikiteketea kutokana na utumiaji wa dawa hizo.
chanzo:Habarileo.
Comments