Shambulio hilo la tarehe 28 mwezi Januari lilikuwa la kwanza lililoagizwa na Bwana Trump.
Bill Owens ambaye mwanawe William Ryan Owen aliuawa, aliambia jarida la Miami Herald kwamba serikali inafaa kumfanyia uchunguzi mwanawe.
''Kwa nini kuwepo kwa ujumbe kama huo wiki moja baada ya yeye kuchukua mamlaka. Kwa nini''? Alisema katika mahojiano na gazeti hilo.
''Kwa kipindi cha miaka miwili hakuna mwanajeshi aliyeruhusiwa kuelekea Yemen, walikuwa wakitumia makombora na ndege zisozokuwa na rubani kutekeleza mashambulio kwa sababu hakukuwa na raia yeyote wa Marekani aliyekuwa akilengwa. Sasa mara moja tunachukua hatua hii''.
Uvamizi huo ulioagizwa na rais Trump siku sita baada ya kuchukua mamlaka unaaminika kuwaua raia kadhaa ikiwemo watoto.
Wamarekani 3 walijeruhiwa katika uvamizi huo uliodaiwa kuanza kupangwa na utawala wa rais Obama.
chanzo:Bbc.
Comments