Wafanyabiashara visiwani Zanzibar wametakiwa kua na utaratibu wa kuhifadhi kumbukumbu katika biashara zao.
Inaonekana baadhi ya wafanyabiashara wengi wao hawajui au kwa makusudi hawaweki kumbukumbu katika shuhuli zao za kibiashara ikiwamo kutotoa risiti hali ambayo inayoifanya bodi ya mapato Zanzibar ZRB kukosa baadhi ya makusanyo kwa wafanyabiashara hao.
Akizungumza na wafanyabiashara hao juzi katika kikao cha kuimarisha mahusiano baina ya ZRB na wafanyabiashara katika ukumbi wa hoteli ya Hifadhi Chakechake Pemba afisa uhusiano wa ZRB Makame Khamis Muhammed amesema kua kutotoa risiti za mauzo kwa ni kosa kisheria hali ambayo inaweza kumfanya mfanyabiashara kuingia katika mkono wa sheria.
Amesema kwa wenye mahoteli na nyumba za kulalia wageni ndio wengi miongoni mwao wasioweka kumbukumbu jambo ambalo hupelekea serikali kutojua ni aina gani ya wageni walioingia nchini na ni kwa kazi gani, hivyo ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kuitika wito wa kutoa risiti kwa kila kunapohitajika kufanya hivyo.
Nao wafanyabiashara hao kwa pamoja wameonyesha kukubalina katika hilo huku wakitoa wito kwa wenzao nchini kufuatasheria ili kujinusuru kujiweka katika hali mbaya kibiashara.
chanzo;zanzibar24.
Comments