Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May
amesema ni wakati sasa nchi yake na Marekani kuanza tena upya
mahuasiano yao maalum na majukumu ya kuongoza pamoja katika kipindi
hiki.
Akizungumza mjini Philadelphia, ikiwa ni mwanzo wa ziara
yake nchini Marekani, ambayo itamuwezesha pia kuwa kiongozi wa kwanza wa
kigeni kukutana na Rais Donald Trump.
Amesema kwa uhakika nchi
yake ambayo imemaliza uanachama wake kwenye Umoja wa Ulaya, iko tayari
kujenga ushirikiano na marafiki zake wa zamani na wapya pia.
chanzo;bbc
Comments