Vijana hao ni sehemu ya waliokwenda kuomba ajira Ikulu mwaka 2015 walijikusanya zaidi ya 500 kutoka nchi mzima katika lango la Ikulu Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti Palale Kiwango ambaye sasa ndiyo kiongozi wa hao waliokwenda kuomba msaada kwa Kamanda Muroto wa kuwatafutia eneo la kulima.
Kamanda Muroto alipata eneo la shamba kwa msaada wa mkazi wa Mtaa wa Lugwadu, Jamila Nzota ametoa sehemu ya shamba lake la ekari 10 na kuwapa vijana hao wanaoendelea na kilimo cha mboga, mbaazi, mahindi na karanga.
Vijana hao 10 kati yao wanawake wanne ambao wanalazimika kwenda na kurudi katika kambi hiyo kutokana na kutokuwepo na sehemu ya kulala ambayo nafasi iliyopo ni kwa wanaume tu.
Mwenyekiti wa wahitimu, Palale Kiwango alisema wameamua kwenda kwa Kamanda Muroto kuomba msaada baada ya kuona kuwa katika maisha siyo lazima kuajiriwa, bora wajiajiri wenyewe kwa kilimo na wanamuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwatembelea na kuwapatia msaada katika kazi hiyo na viongozi wa serikali, watu binafsi, taasisi na mashirika mbalimbali ya nchini na kimataifa wawasaidie.
Vijana hao wamemshukuru Kamanda Muroto kwa kuwaonesha njia ambayo kwao ndiyo itakuwa mkombozi wa maisha yao na kuwataka vijana wengine wasing’ang’anie ajira watafute njia nyingine au fursa ambazo zipo nyingi.
chanzo;habarileo.
Comments