Rais wa Gambia atangaza hali ya hatari.

Yahya Jammeh aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi mwaka 1994Rais yahya Jammeh wa Gambia ametangaza hali ya hatari baada ya kukataa kuondoka madarakani kufuatia kushindwa kwenye uchaguzi uliofanyika Disemba mwaka jana.

Rais Jammeh ametangaza hali ya hatari hapo jana na kusema inaanza kutekelezwa mara moja na itadumu kwa siku tisini. Katika tangazo hilo, rais Jammeh amelaumu nchi za nje kuingilia masuala ya ndani ya Gambia, baada ya machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imemtaka rais Jammeh, ambaye aliingia madarakani mwaka 1994, kuheshimu matokeo ya uchaguzi huo na kuachia madaraka kwa rais mteule Adam Barrow, ambaye hivi sasa yuko Senegal.

chanzo;cri.

Comments