Wakazi wa mji huo wameonekana wakishangilia wakati msafara wa wanajeshi hao ulipokuwa ukipita.
Aliyekuwa
Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh aliondoka mapema siku ya jumapili
ikiaminika kuwa amepewa hifadhi nchini Gine ya Ikweta.
Jammeh
ambaye alishindwa uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka jana, ameondoka
madarakani baada ya kuwepo shinikizo kutoka jumuia ya kiuchumi ya nchi
za Afrika magharibi, ECOWAS.
Raia wa Gambia wameeleza kile walichodai kuwa ahueni kwa hali ilivyo hivi sasa..na namna walivyofikia tamati kwa amani.
''leo
nina furaha, Ndio, kwa sababu Rais Jammeh ameondoka.Sasa kila mtu
ametulia, wana furaha leo, nina furaha sana sana'' alieleza raia mmoja.
chanzo;bbc.
Comments