Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini Unguja, wakati akizungumza na Zanzibar 24 huko ofisini kwake Tunguu Wilaya ya Kati Unguja, alisema wanaotafutwa ni Saidi Ali, Suwedi na Maryam wote wakaazi wa Jumbi mkoa wa kusini Unguja.
Alisema watuhumiwa hao wote kwa pamoja walimshambulia Catherina Saidi Yohana (22) mkaazi wa Jumbi kwa kumpiga mikwaju ya mgongo na mdomoni hali iliyomsababishia kupata maumivu ya mwili.
Aidha alisema, mabali na kipigo hicho watuhumiwa hao pia waliukata mkufu wa shingoni dada huyo pamoja na lakti yake ambavyo thamani ya vitu hivyo ni shilingi 8000.
Jeshi la polisi linaendelea na kuwatafuta watuhumiwa hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
chanzo:zanzibar24.
Comments