Mtoto achomwa moto akidaiwa kuiba 10,000/-.

motoMtotomwenye umri wa miaka 7 amelazwa katika hospitali ya micheweni baada ya kupata majeraha ya kuchomwa moto kwenye mikono na mjomba wake aliyefahamika kwa jina la Hamad Juma Shineni mkaazi wa chamboni micheweni.
Taarifa zilisema mtoto ambae ni yatima alifikwa na kadhia hiyo baada ya kutuhumiwa kuiba shilingi 10,000/- za mjomba ake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta kijan aliefanya kitendo hicho ili akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Nae dakatari wa zamu wa hospitali ya Micheweni Khalfan Salim Said aliwataka wananchi kujitokeza kumsaidia mtoto huyo ili aweze kupata matibatu ikiwemo sindano ya tetnus ambayo imekosekena hospitalini hapo.
Amesema hali ya afya ya mtoto huyo inaendela vizuri kutokana jitihada walizozichukua za kumsaidia mtoto huyo .
Nae afisa ustawi Wa jamii Wilaya ya Micheweni, Hamad Masoud alikilaani kitendo hicho na kuvitaka vyombo vya sheria kuchukua hatua dhidi ya mtuhumiwa huyo.
 chanzo;zanzibar24.

Comments