Mfumo wa kisiasa Zanzibar changamoto kubwa kwa asasi za kiraia.

asasiAsasi za kiraia Zanzibar zimetakiwa kujijengea mazingira bora  katika ufanyaji wa kazi zake za kuisaidia jamii  licha ya kuwa  zinakabiliwa na matatizo mengi yanayokwamisha jitihada zao za maendeleo.

Akizungumza katika mkutano  huo uliokutanisha  asasi mbalimbali Zanzibar mkufunzi wa chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)Dr.Issa Haji Zidd amesema bado  asasi nyingi zinakabiliwa na matatizo  na  kurudisha nyuma malengo kutokana na  kukosa msukumo wa pamoja kati ya asasi na wawekezaji  ukosefu wa utaalamu na ushirikiano mdogo  kwa wanaasasi.

Mkufunzi huyo amesema asasi  za kiraia  duniani kote zimekua na mchango mkubwa katika shughuli mbali mbali za kijamii na serikali hivyo ni vyema asasi hizo kuthaminiwa.

Amesema   katika kuthamini asasi hizo Serikali ya mapinduzi Zanzibar wameweka utaratibu maalumu wa kuzitambua asasi hizo ikiwa ni pamoja na kuzipatia usajili rasmi.

Alizikumbusha asasi hizo majukumu yao ni pamoja na kuhakikisha wanazisaidia jamii katika  kukabiliana na changamoto zikiwemo kupambana na umaskini  pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake.

Mtoa mada  Hassan Jani Masoud amesema licha ya uwepo wa asasi mbali mbali ambazo zimekuwa na mchango mkubwa kwa serikali bado asasi hizo zinakabiliwa na  matatizo  mengi   katika utendaji wa kazi zake.

Akitaja miongoni mwa matatizo  hayo Hassan amesema mfumo wa kisiasa Zanzibar unaleta changamoto kubwa kwa asasi za kirai katika kufanya kazi kutokana   kukosa uhuru wa kufanya kazi  na kupata ugumu  kwenye kutekeleza majukumu yao.
chanzo:zanzibar24

Comments