KAIMU KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT JUMA MALEWA AFANYA MABADILIKO YA UONGOZI KWA MAAFISA WAANDAMIZI WA MAGEREZA.
Mabadiliko hayo ni pamoja na
aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Magereza SACP Katos Rugainunura amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza
sehemu ya Utawala na nafasi yake inakaimiwa na Kamishna Msaidizi wa
Magereza ACP Mzee Nyamka aliyekuwa Mkuu wa Utawala Magereza Mkoani
Morogoro. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Antonino Kilumbi
aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma amehamishwa kwenda Makao
Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kikosi cha Ujenzi na nafasi yake
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Julius
Sang’udi aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya.
Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa
wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Anderson Kamtiaro
anaenda kuwa Afisa Mnadhimu Magereza Mkoani Arusha na nafasi yake
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Hassan Mkwiche ambaye
alikuwa ni Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Gereza
Same Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Evarist Katego anakwenda kuwa
Mkuu wa Gereza Kuu Karanga, Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Uwesu Ngarama
amehamishiwa Makao Makuu kuwa Boharia Mkuu wa Jeshi na nafasi yake
inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mipango wa Jeshi ACP Athuman Kitiku.
Aidha, aliyekuwa Mkuu wa
Magereza Mkoani Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Musa Kaswaka
anakwenda Makao Makuu Kitengo cha Ukaguzi na nafasi yake kuchukuliwa na
Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Ismail Mlawa aliyekuwa Mkuu wa
Kiwanda cha Samani Gereza Kuu Ukonga. Aliyekuwa Afisa Mdhibiti wa Fedha
wa Jeshi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP Gideon Nkana
anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga, Dar es
Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP
Chacha Jakson.
Wengine ni pamoja na aliyekuwa
Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Mbeya ACP Kijida Mwakingi anakaimu
nafasi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza
ACP Abdalah Misanga anayetoka Gereza Mgumu kwenda kuwa Mkuu wa Gereza
Msalato, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP John Itambu anayetoka Gereza
Kilosa kwenda kuwa Mkuu wa Kiwanda cha Samani Gereza Kuu Ukonga.
Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP
Erasmus Kundy anayetoka Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga kwenda
Makao Makuu Kitengo cha Habari, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Julius
Ntambala aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi Makao Makuu anabakia
Makao Makuu Kitengo cha ujenzi kuwa Msaidizi wa Mkuu wa Kitengo,
Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Sylivester Mrema anayetoka Gereza
Idete kwenda Gereza Ubena kuwa Mkuu wa Gereza.
Aliyekuwa Mkuu wa Gereza Ubena
Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Shaba Zephania anakwenda Magereza Mkoa
wa Pwani kuwa Afisa Mnadhimu, Kamishna Msaidizi wa Magereza ACP Solomon
Urio anayetoka Makao Makuu kwenda Magereza Mkoa wa Dar es Salaam kuwa
Afisa Mnadhimu pamoja na aliyekuwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza SACP George Kiria amehamishiwa
Makao Makuu Kitengo cha Uhasibu .
Mabadiliko hayo ni ya kawaida na yanalenga kuboresha utendaji kazi na ufanisi wa Jeshi la Magereza.
Imetolewa na
Lucas Mboje – ASP
Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza
Makao Makuu ya Magereza Tanzania Bara.
CHANZO: fullshangweblog.
Comments