Akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la tatu la Biashara lenye lengo la kuendeleza shamrashamra za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar huko Maisara Dk. Shein amesema mataifa mbalimbali yanaimarika kimaendeleo kutokana na wananchi wao kuimarisha ushirikiano katika kushiriki matamasha ya biashara yanayotoa fursa ya kutangaza biashara kwa Nchi jirani.
Hata hivyo amesema katika kuzalisha bidhaa zinazoendana na mahitaji nchi serikali inaendelea na utoaji elimu kwa wajasiria mali ili kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazoendana na mahitaji pamoja na kuinua uchumi wa nchi.
Akizungumzia suala ukiukwaji wa sheria ya kuingiza biashara nchi Dk.Shein amesema serikali itahakikisha inawachukulia hatua za kisheria wafanya biashara wanaoingiza biashara kinyume na sheria walizowekewa ikiwemo kuingiza biashara zilizopita muda wa matumizi pamoja na kukwepa kulipa kodi jambo linalopelekea kuikosesha serikali mapato ya kodi za biashara hizo.
Kwa upande wake Waziri wa Biashara viwanda na Masoko Zanzibar Balozi
Amina Salum Ali amesema mbali na wafanya biashara kulitumia tamasha hilo
kwa kutangaza biashara zao pia tamasha hilo litasaidia kuinua soko la
utalii pindipo wafanya biashaa ,Taasisi binafi na za Serikali kuungana
pamoja katika kutangaza biashara zao.
Jumla ya wafanya Biashara 150 wameshiriki tamasha la tatu lilofunguliwa huko maisara ambalo limeshirikisha wafanya biashara wa sekta mbalimbali na linatarajiwa kudumu kwa muda wa siku saba.
chanzo: Zanzibar24
Comments