Barrow aliapishwa wiki iliyopita nchini Senegal wakati viongozi wa kieneo walipokuwa wakimshawishi Jammeh kuondoka madarakani.
Maelfu ya watu walifurika katika barabara za mji mkuu wa Gambia Banjul kumlaki rais huyo mpya.
Wanadiplomasia walimtaka Barrow arudi mara moja nyumbani kuepuka pengo la uongozi.
Taarifa zinasema Barrow atakaa katika makaazi yake wakati ukaguzi
ukifanywa katika ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa
Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.
Maelfu kadhaa ya
wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi wanasalia Gambia wakati kukiwa
na taarifa kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya
usalama nchini.
chanzo:bbc.
Comments