Takribani Wanafunzi 25 na Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ya Unberkant huko Ruvuma wamejeruhiwa baada ya kupigwa na radi iliyokuwa imeambatana na mvua kali.
Imeripotiwa kuwa radi hiyo pia imeharibu mfumo mzima wa umeme katika shule hiyo ya sekondari ya Unberkant. Aidha wanafunzi wengine watatu hali zao ni mbaya na hospitali wanaendelea na matibabu.
Comments