Sherehe za kutiliana saini makubaliano hayo zilifanyika katika ofisi
za eneo tengefu Saateni na ZSTC iliwakilishwa na Mkurugenzi Mwendeshaji
Dkt. Said Seif na Kampuni ya Genefryd iliwakilishwa na Afisa wake Bw.
Pale Christeusen.
Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo, Dkt. Said amesema
Zanzibar imekuwa ikifanya biashara ya karafuu kwa miaka mingi lakini
hivi sasa itapanua wigo wa kuuza karafuu hai Ulaya na kupata faida
kubwa.
Alisema Ili Zanzibar iweze kutoa karafuu hai tahadhari kubwa inapaswa
kuchukuliwa wakati wa kuotesha miche, ukuaji wake na kufikia wakati wa
kuzaa bila ya kuingizwa aina yoyote ya mbolea zenye kemikali.
Ameongeza kuwa uangalizi mkubwa pia unahitaji katika mchakato mzima
wa kushughulika kilimo hicho kuanzia hatua ya kuchuma, kuanika,
kuzihifadhi mpaka kuzisafirisha hivyo amewaomba wananchi kuunga mkono
kuingia katika kilimo hai kwa vile karafuu ndio tegemeo lao na Taifa kwa
jumla.
Amesema sambamba na kuanzisha kilimo hai cha zao la karafuu
Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC amewataka wananchi kuendeleza zao hilo
katika mfumo wa kawaida kwa kuongeza upandaji miche na kuacha tabia ya
kukata mikarafuu kwa ajili ya kuni, kufanyia mkaa na kujengea.
Bw. Christeusen amewashauri wakulima wa karafuu Zanzibar kuongeza
kilimo hai cha karafuu kwa vile kinafaida kubwa katika soko la Ulaya.
chanzo; zanzibar24.
Comments