ZSSF yakabidhi msaada kuboresha huduma za usafi hospitali ya Mnazi mmoja.

Mfuko wa hifadhi ya jamii (ZSSF) umekabidhi jumla ya madastibini 43 ya kuhifadhia taka katika hopital kuu ya mnazi mmoja ikiwa ni miongoni mwa harakati zao za kusaidia jamii.

Akikabidhi madastibini hayo yenye thamani ya shilingi milioni 3 katika hospitali ya Mnazi mmoja afisa msaidizi wa masoko na mahusiano wa (ZSSF) Khatibu Iddi amesema,mfuko huo upo kwa ajili ya kusaidia jamii hivyo wametoa msaada huo kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa usafi na kuzuia maambukizi kwa watu wanaofika hapo.

Kwa upande wake katibu msaidizi wa hospitali ya mnazi mmoja Abubakar Khamis Hamad ameipongeza (ZSSF)  kwa kutoa msaada huo na kuitaka jamii kuyatumia madastibini hayo kwa mujibu wa maelekezo na kuwataka kuwa na mashitikiano ili kutunza mazingira na kuondoa magonjwa ya maambukizi yanayoweza kujitokeza.

Nae muuguzi mkuu wa hospitali ya Mnazi mmoja Margaret Tayari ametoa wito kwa jamii kuwasaidia katika kuboresha usafi katika hospitali hiyo na kuwataka kuzitenganisha taka kwa kujibu wa maelekezo ili kusaidia kusanifu taka hizo kupitia mtambo wao wa kusanifia.

Amesema ” dastibini jekundu ni la taka hatarishi, dastibin la manjano nilataka za karatisi na dastibini la bluu n la taka za vyakula vyakula”

chanzo;zanzibar24.

Comments