Watatu wafariki kwa ajali ya gari.

Watu watatu akiwemo raia wa kigeni wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya gari za kuchukua wageni kugongana uso kwa uso  katika eneo la Mungoni mkoa wa Kusini Unguja.
Akizungumza na ZANZIBAR24 juu ya ajali hiyo kamanda wa polisi wa mkoa huo Juma Saad amesema madereva wote wawili wa gari hizo pamoja na abiria mmoja raia wa India wamefariki dunia.
Kamanda Saad amewataja waliofariki ni Seif  Khamis Ali miaka 27 mkaazi wa Jango’mbe, Hassan Suleima miaka 50 mkaazi wa Kidoti na Shekizari Shakarolola raia wa India.
Waliojeruhiwa ni mke wa Marehemu Shakarola raia wa India na Husna Hassan Zahor miaka 16 na wote wamelazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja.
Aidha Kamanda Saad amewataka madereva kuendesha gari kwa mweno wa pole kutokana na barabara nyingi za Zanzibar ni nyembamba na zenye mashimo.

 chanzo:zanzibar24

Comments