Akizungumza na Zanzibar24 huko ofisini kwake Mombasa Mkuu wa Biashara na uwendeshaji wa bodi hiyo Adbul aziz saidi Muhammed amesema mbali na elimu wanayopewa wafanya biashara juu ya kuingiza bidhaa zilizokuwa na viwango lakini baadhi yao wanakiuka sheria hiyo.
Hata hivyo amesema, wafanya biashara wanajukumu la kufata masharti ya kiafya yaliowekwa pamoja na kukubali biashara zao kufanyia uchunguzi kabla ya kusambazwa kwa watumiaji.
Aidha abdul azizi ametowa wito kwa wananchi kuripoti matukio ya uingizwaji wa bidhaa za vyakula vinavyoingizwa kinyume na sheria ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo maradhi ya kensa.
Kwa mijibu wa kauli ya Bodi ya Chakula dawa na vipodozi Zanzibar imesema zaidi ya viwanda vinane kutoka nchi mbali mbali ikiwemo Brasil,China ,Oman na Rashia vinavyoingiza biashara nchi Tanzani vimekaguliwa vimeruhusiwa kuleta bidhaa zao Tanzania baada ya kutimiza masharti ya kiafya yanayohitajika katika bidhaa..
CHANZO;zanzibar24.
Comments