
Akizungumza na Zanzibar24 Kaimu Afisa Sheria Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni Ali Abdalla Haji amesema endapo wananchi watajitokeza katika uwekaji wa pingamizi kwa baa hizo itaweza kusaidia kuziondosha baa hizo zinazowaletea matatizo na usumbufu.
Hata hivyo amesema licha ya Halmashauri kutoa elimu katika wadi na shehia za wilaya hiyo juu ya kujitokeza kupinga lakini muamko umekuwa mdogo na hivi sasa imeonekana wananchi wamegoma kupinga baa.
Kwaupande wao baadhi ya Wananchi Wameiyambia Zanzibar24 kuwa hawatojitokeza kupeleka pingamizi zao katika Mahakama ya Vileo kutokana na kuvunjika moyo kwani malalamiko yao kutofanyiwa kazi licha ya kujitokeza kwa wingi kila mwaka.
Jumla ya baa baa 20 zimepeleka maombi ya kupatiwa lessen kwa mwaka 2017 katika Wilaya ya kaskazini B.
CHANZO; Zanzibar24
Comments