
Ushauri huo
umetoleawa na Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Salama Mbarouk Khatib wakati
akizungumza na wafanya biashara hao huko katika ukimbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Kusini Pemba.
Amesema ni
jukumu la kila mmoja kuchangia madawati na sikwawafanya biasha pekee bali kila
mtu linamgusa kwani wanafunzi wanaopatashida maskulini niwao wenyewe.
"Najua
hatuna uwezo wa kununua madawati lakini tukishirikiana kwa pamoja tunaweza
kupunguza uhaba huu uliopo kwa sasa"
Ameeleza kuwa
ili elimu imfikie mwanafunzi vizuri, nilazima jukumu la kuhakikisha anapatiwa
makazi mazuri yatakayo mjenga katika kujiendeleza kielimu nakuweza kujiandalia
mazingira mazuri ya kujisomea.
Amaefahamisha
kua katika kuipa msukumo sekta ya elimu wadau mbali mbali wakiwemo wafanyabiashara pamoja na wengineo kujitolea kwa hiari
kuchangia madawani kwani kwa sasa imekua kero kwa skuli nyingi hapa nchini.
Amesema ili kuondokana na changamoto za
madawati katika skuli zetu hapa nchini nilazima kila mmoja wetu kuunganisha nguvu za pamoja kujitolea kwa halia na mali kwania ya kutokomeza kero hizo zisienee.
"Naaimani
sote hatuna uwezo kwani dawati moja linauzwa 350000 lakini tukiwa na nia moja
tunaweza"
Kwa upande
wao wafanya biashara wa chake chake wamemuhakikishia mkuu huyo wa wilaya kuwa wapo tayari kuchangia madawati kwa
maendeleo ya wanafunzi hususana katika skuli amabazo zinaonaupungufu wa kwani
kila mmoja anahaki ya kujisomea akiwa mazingira mazuri.
Comments