Vuai Ali Vuai; CCM inahitaji viongozi wabunifu kutekeleza ahadi zake.

Zaidi ya shilingi milioni 43 zimetumika kununua gari ya mizigo na dawa za binadamu kwenye vituo vya afya vya jimbo la Chumbuni ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na uongozi wa jimbo hilo wakati wa kampeni za uchaguzi.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa wananchi wa jimbo hilo Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai  amewataka wananchi wa jimbo hilo kunga mkono huhudi za maendeleo zinazofanywa na viongozi wao.
Amesema chama hicho kwa sasa kinahitaji viongozi wabunifu wenye uwezo wa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 bila ya kusukumwa kwa lengo la kutatua matatizo ya wananchi.
Nae mbunge wa Jimbo hilo, Ussi Salum Pondeza amesifu ushirikiano uliopo kati yake, wananchi na viongozi wengine wa Jimbo hilo na kuahidi kuwa wataendelea kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi
Katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi miwili iliyopita uongozi wa jimbo hilo umetumia zaidi ya shilingi milioni 205 kwa shughuli za kutatua  matatizo yanyowakabili wananchi wa jimbo la Chumbunio.
 chanzo;zanzibar24

Comments