Upotevu wa Faru John wawatia utatani maafisa wa hifadhi ya Ngorongoro.

johnWaziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kutoa ufafanuzi kuhusu kuhamishwa kwa faru maarufu kwa jina la John kutoka kwenye hifadhi hiyo.
Bw Majaliwa amewataka viongozi wa NCAA kuwasilisha kwake nyaraka zote zilizotumika katika kumuhamisha faru huyo kufikia Alhamisi.
Alisema ana taarifa kuwa faru huyo John alihamishwa kwa siri na kupelekwa Grumeti katika eneo Serengeti mnamo 17 Desemba, 2015.
“… mliahidiwa kupewa shilingi milioni 200 ambapo mkapewa shilingimilioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa shilingi milioni 100 nyingine baadaye,” alisema Bw Majaliwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania, Bw Majaliwa alisema kwa miezi mitatu sasa, hakuna taarifa zozote kumhusu faru huyo ambazo zimetolewa.
“Naomba niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,”.

Comments