Uchaguzi Dimani Januari 22.

dsc_0647Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchukuaji fomuza kujaza nafasi zilizo wazi ya mbunge na madiwani katika maeneo mbalimbali nchini.
Imesema inatarajia kuendesha uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani mkoa wa mjini magharibi , kufuatia kifo cha aliyekua mbunge wa jimbo hilo Hafidh Ali Twahir.
Marehem Hafidh  alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 11 katika hospitali ya General iliyoko mkoani Dodoma alikokua amekwenda kushiriki shughuli zake za kikazi.
Hivyo taarifa kuhusa uchaguzi huo iliyotolewa jana jijini Dar es salaam na tume hiyo, hatua hiyo inatokana na vifungu vya 37 (1) (b) na 46 (2) vya sheria ya tume ya uchaguzi, sura ya 343 na  vifungu vya 13 (3) na 48 (2) vya sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa, sura 292.
Aidha tume hiyo pia itaendesha chaguzi nyengine ndogondogo za kujaza nafasi za wazi za udiwani katika kata 22 kwenye baadhi ya halmashauri za Tanzania bara zilizokua wazi kutokana na sababu mbalimbali.
Tume hiyo imesema kuwa zoezi la kuto fomu za uteuzi litaanza Disemba 10 hadi 22 na kufuatiwa na zoezi la uteuzi wa wagombea, Disemba 23 hadi Januari 21mwakani itakua ni kipindi cha kampeni  ambapo Januari 22 mwakani itakua ni siku ya kupiga kura.
chanzo;zanzibar.

Comments