Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar yawataka wananchi kwenda kuhakiki waliofariki.

zecKwa Mujibu wa Tangazo kutoka katika tovuti ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar: Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imetoa orodha ya waliofariki na kubandika orodha hizo katika ofisi za tume ya uchaguzi katika wilaya zote za Unguja na Pemba.
Hivyo Tume inawataka wananchi kwenda kuangalia orodha hizo ili kama kuna kasoro zozote wanapaswa kuweka pingamizi kwa lengo la kunusuru kufutwa kwa walio na sifa.
Orodha hizo zimeekwa tangu tarehe 5/12/2016 na mwisho wa kwenda kutizama ni tarehe 12/12/2016.
 chanzo;zanzibar24.

Comments