Mbunge
wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu jana
aliwaomba radhi wakazi wa Mbeya, wanafamilia, ndugu wa marehemu Recho
Lutumo (14) aliyefariki dunia baada ya kugongwa na gari lake juzi.
Ajali
hiyo ilitokea wakati gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Gabriel
Andrew (43) mbunge huyo akiwamo lilipokuwa likitoka jijini hapa kwenda
Uwanja wa Ndege Songwe (Sia).
Recho
ambaye ni yatima na aliyekuwa akilelewa na bibi yake Neema Lutumo,
aligongwa wakati akivuka kwenye alama za watembea kwa miguu eneo la
Iyunga katika barabara kuu ya Zambia.
Sugu
akiwa na baadhi ya viongozi wa Chadema jijini Mbeya alishiriki
maandalizi na shughuli zote za mazishi ya mtoto huyo kuanzia nyumbani
ambako ndiko alikoomba radhi.
chanzo;mpekuziblog.
Comments