Serikali yashauriwa kulipatia ufumbuzi tatizo la Walimu wa Madrasa kutolipwa.

Holy-QuranSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshauriwa kulipatia ufumbuzi wa haraka tatizo la kutolipwa walimu wa madrasa ili waweze  kunufaika na elimu wanazotoa kwa wanafunzi.
Akizungumza na Zanzibar24 nje ya maulidi ya Kumswalima Mtume Muhammad (S.A.W) katika madrasa ya kadiria B huko Bububu  Mkuu wa Chuo cha kiislamu Zanzibar Dk.Muhidin Ahmad Khamisi amesema  mbali na walimu wa madrasa kujitolea katika kuwasomesha wananfunzi lakini wamekuwa wanakosa malipo maalum kulinganisha na elimu zao.
Hata hivyo ametoa wito kwa wadau wa maendeleo  kuwa mstari wa mbele katika kusaidia elimu ya dini ya kiislamu  kutokana na baadhi ya madrasa kuwa katika hali isiyoridhisha  juu ya kutoa elimu bora kwa wananfunzi.
Akizungumza katika maulidi hayo Mwakilishi wa Jimbo la BUBUBU Masud Abdul Rahman amesema mbali na matitizo yanayowakumba walimu na wananfunzi katika kutafuta elimu ya dini ya Kiislamu laiki pia wanajukumu la kutunza maadili ya kiislamu ili kulinda utamaduni uliopo nchini.
chanzo; Zanzibar24

Comments