Serikali kuelekea kupandisha kodi nishati ya mkaa.

mkaaSerikali imesema kuwa inakusudia kupandisha kodi ya Nishati ya Mkaa ili kudhibiti ukataji miti hovyo ambao unasababisha ukame na joto.

Serikali inachukua hatua hiyo baada ya kuona asilimia 93 ya Watanzania ni watumiaji wakubwa wa Nishati ya Mkaa na Kuni.

Waziri Prof. Maghembe amesema ukataji miti unatishia uhai wa Watanzania kutokana na ukweli kwamba ukataji miti unasababisha ukame na joto. “Nafikiri tukipandisha kodi ya mkaa, lazima utapanda bei maradufu na hivyo idadi ya watu wanaokata miti kwa ajili ya uuzaji wa mkaa itapungua, hapo tutakuwa tumeokoa misitu yetu” alisema Maghembe.

chanzo; zanzibar24.

Comments