Taarifa hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, ambapo amesema kuwa
makato kiwango hicho kimepanda kutoka asilimia 8 ya sasa.
“Hii asilimia 15, kimsingi sheria ninavyofahamu ilishasainiwa, baada
ya hapo kuna kuiangalia iendane na kanuni zetu, baada ya kuicheki
imeendana na kanuni zetu kama kuna sehemu itahitaji kuboreshwa kidogo
haitazidi miezi miwili au mitatu, baada ya hapo tutaweza kutumia hiyo
15%, na asilimia 15 ya safari hii ni tofauti na siku za nyuma, siku za
nyuma tulikuwa tunachaji asilimia 8”, amesema Manyanya.
Hapo awali wadaiwa hao wa mikopo walikuwa wanakatwa asilimia 8,
lakini sheria ya sasa itaruhusu wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu
kukatwa asilimia 15 ya kipato chao.
Pia Manyanya amesisitiza kuwa kwa wale ambao hawajaajiriiwa, lakini
wanafanya biashara zao wanatakiwa kuwasilisha angalau shilingi 120,000
kila mwezi na kuwashauri kuwa ni vema wakapeleka zaidi ili wamalize
haraka madeni yao.
Kuhusu wasio na kazi, amesema haiwezekani mtu asome halafu akose
shughuli ya kufanya na kuwataka kutafuta shughuli yoyote ya kufanya ili
waanze mapema kulipa madeni yao ndani ya miaka miwili baada ya kuhitimu
masomo.
chanzo; zanzibar24.
Comments