Mwanafunzi
wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo Meru mkoani
Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na kutelekezwa kwenye
korongo la mchanga na kusababishiwa maumivu makali yaliyomsababishia
kushindwa kuendelea na masomo yake kwa muda.
Akielezea
tukio hilo mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za
kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa
12:30 alipotoka kwa kinyozi.
Alisema
kuwa ghafla akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu aliyemfanyia
kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili asitoe
sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili ambacho
kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.
“Nilijitahidi
sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa amenikaba shingoni
alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho kimenipelekea nishindwe
kuendelea na masomo yangu kwani baada ya vipimo nimeonekana aliniumiza
sehemu nyingi ikiwemo hata kifua changu,” alisema mwanafunzi huyo.
Kwa
upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli
Akyo alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti
zao ni vema Serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika kwani
tangu akamatwe mtuhumiwa huyo na kupelekwa kituoni bado hajasomewa
shtaka linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na vitendo hivyo kuona
wako sawa kwa vile hakuna hatua kali inayochukuliwa mapema dhidi ya
matukio hayo
Nae
mkuu wa shule hiyo Nkoe Nicolaus alisema kuwa tukio hilo limemfanya
mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili huo
ameshindwa kiendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri wazazi wa
binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumpeleka sehemu nyingine jambo
ambalo litamsaidia kurudi katika hali yake ya awali.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu Tanesco, Samweli Matayo
alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na kusema kuwa
mara baada ya taarifa kutolewa walifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa
aliyetambulika kwa jina la Wilson Elias ambae ndie aliyehusika na
ukatili huo na kumfikisha katika kituo kidogo cha Polisi Usa River ili
kukabiliana na shutuma hizo.
Kamanda
wa Polisi, Charles Mkumbo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na
kusema kuwa mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016 na
atafikishwa mahamani upelelezi ukikamilika.
chanzo;mpekuziblog.
Comments