mwaka 1 jela kwa wizi wa pikipiki.

dhamanapic-1MAHAKAMA ya Wilaya Chake Chake, imewahukumu washitakiwa wanne, kutumikia kifungo cha miezi kumi na mbili jela, baada ya kubainika na kosa la wizi wa Pikipiki aina ya Freedom Prima, yenye thamani ya shilingi 2,220,000.
 
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu wa mahakama hiyo, Ahmed Jumbe Marika chini ya kifungu 311 sheria namba 7 ya mwaka 2004, kutokana na kuwa mshitakiwa namba mbili Hassan Khamis Rashid (18), anakabiliwa na kosa kama hilo, na yupo jela anatumikiwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi sita.
 
“Kutokana na madai ya upande wa mashitaka kuwa mshitakiwa namba mbili, anatumikia chuo cha mafunzo, hivyo mahakama imewapunguzia adhabu chini ya kifungu 311 sheria namba 7 ya mwaka 2004 wote kwa pamoja kutumikia kifungo cha mwaka mmoja badala ya miaka mitatu.
 
Akisoma shitaka hilo, mwendesha mashitaka wa mahakamahiyo Mohamed Ali Juma alisema mbele ya washitakiwa hao kuwa shitaka lao lipo kwa ajili ya hukumu ingawa wenzao wawili hawakufika mahakamani bila ya taarifa zozote.
 
“Muheshimiwa hakimu shitaka hili lipo mbele yako kwa jaili ya kutolewa hukumu dhidi ya washitakiwa, ila kutokana na washitakiwa wawili ambapo ni mshitakiwa nambari tatu na namba nne hawakufika mahakamani na hakuna sababu za msingi ama, taarifa zozote ni vyema mahakama ikaangalia kwa kina na kutoa hukumu inyofaa dhidi yao ili iwe fundisho kwao na wa wengine,”aliiambia mahakama mwendesha mashitaka huyo.
 
 Washitakiwa hao Abeid Khamis Abeid (29), Hassan Khamis Rashid (18), Ibrahim Burhan Yussuf (23) na Mohamed Sharif Mohamed (37) wote kwa pamoja mnamo Septemba 8 mwaka 2015, majira ya saa 4:15 usiku, Msikiti Kitibegi Wawi Chake Chake, waliiba Piki piki aina ya Freedom Prima 125 yenye namba ya usajili 2609 DM yenye thamani ya shilingi 2,220,000 mali ya Said Mohamed Sadik.
 
Kosa la Wizi ni kinyume na kifungu 274 (1)cha sheria nambari 6 ya mwka 2004 jambo ambalo ni kosa kisheri
 
chanz ;zanzibar24.

Comments