Amesema kuwa maneno yaliotolewa na kijana
huyo ni ya dharau kwa Mwenyezimungu na udhalilishaji kwa mtume Muhammad
pamoja na waislamu wote ni maneno ambayo hayawezi kupuuzwa bila ya
kuchukuliwa hatuaza kisheria.
Ameyasema hayo huko ofisini kwake
mazizini wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya udhalilishaji
wa matamshi kwa Allah (S.W)pamoja na Mtume wake yaliotolewa na Abdallah
Saleh.
Sambamba na hayo ametoa onyo kwa waumini
wa dini ya kiislam kutotamka maeno kama hayo kwa kuendekeza nafsi zao na
kufikia kumtusi Mtume Muhammad(S.A.W) na kutoka kwenye twaa ya
Mwenyezimungu (S.W) kwani kufanya hivyo kunapelekea kupata laana za
Allah na Mtume wake.
chanzo: Zanzibar24.
Comments