Mapaparazi Nungwi wawasumbua watalii.

Wafanyabiashara wanaouza bidhaa za kitalii pembezoni mwa fukwe za bahari ya Nungwi wanadaiwa kuleta usumbufu mkubwa kwa watalii wanaofika kutembelea kijijini hapo kwa ajili ya kupumzika.
Uchunguzi uliofanywa na Mwanahabari wetu umegundua kuwa  wafanyabiashara hao marufu mapapazi wanavibali vya kufanya biashara katika maeneo hayo waliodai wamepewa na ofisi za halmashauri.
Akizungumza na Zanzibar24 mmoja wa wafanyabiashara hao amesema wanafanya biashara katika maeneo hayo baada ya kuruhusiwa na kupewa kibila kinachomruhusu kufanya biashara katika maeneo hayo.
Akizungumza  juu ya tatizo hilo Mkurugenzi wa masoko kutoka kamisheni ya utalii Zanzibar Miraj Ukuti Ussi amesema serikali inawashajihisha wananchi kuzitumia fursa za utalii kufanya biashara katika maeneo yanayokubalika kisheria.
Amesema kufanya biashara kwenye fukwe ni kinyume cha sheria zinazoongoza sekta ya utalii kutokana na kuleta kero kwa watalii wanaofika kwenye hoteli kwa kupumzika.
Sekta ya utalii Zanzibar inaingiza asilimia 75 ya fedha za kigeni ikilinganishwa na serkta nyingine na mwaka huu zaidi ya watalii laki moja na elfu 80 waliwasili nchini.
chanzo;zanzibar24

Comments