Maofisa wadhamin Pemba wakumbushwa kufanya kazi kwa bidii.

Image result for pemba islandNa Asha Salum.
OFISA Mdhamin Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Pemba, Sihaba Haji Vuai, amewataka maofisa wa Wilaya Kisiwani Pemba, kufanyakazi kwa kufuata ratiba zinazotambulika kisheria, ili kurahisisha utendaji wa shughuli zao.
Ameyasema hayo katika mkutano na maofisa hao, huko Chamanangwe, Wilaya ya Wete wakati alipokuwa akiwaelekeza utaratibu wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma.
Amesema kuwa, watumishi wa umma ni lazima watekeleze shuguli zao kwa utaratibu maalum unaotambulika na wanajamii anaowatumikia jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa matatizo yanayoweza kujitokeza.
SaAidha amewataka watumishi hao, kutoa taarifa kwa wakati zinapotokezea zarura za kutofika katika eneo la kazi, ili kusaidia urahisi wa upatikanaji wa huduma na taarifa.
Hata hivyo amewasisitiza, watumishi hao, kufanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja na sekta nyengine za Serikali jambo ambalo litasaidia kupata mafanikio katika kazi zao, huku akiwaahidi kuyafanyia kazi matatizo yanayorejesha nyuma juhudi zao hatua kwa hatua kila hali itakaporuhusu.
Wakichangia katika mkutano huo, maofisa hao, walisema kuwa, sambamba na ufuataji wa ratiba wamekuwa wakikwazwa na usafiri wa kufikia katikamaeneo kwa wakati unaohitajika.
Kwa upande wake, Ofisa Mifugo Wilaya ya  Mkoani, Abdalla Hamad Khamis, amesema kuwa ni vigumu kufuata ratiba katika utekeleaji wa shughuli za mifugo kutokana na muingilianao wa matukio katika maeneo tofauti.
Kwa upande wake, Ofisa Uvuvi Wilaya ya Micheweni, Mzume Juma Faki, amewataka maofisa wenzake kuongeza bidii ya kazi kwa kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli zao, ili kwenda samba na maagizo ya utumishi kwa umma.

Nae Ofisa Mkuu wa Uendeshaji na Utumishi, Issa Nassor Bakar, amewaasa watumishi hao kuwatumikia wanajamii kwa moyo mmoja kwa kufuta taratibu na kanuni za kisheria, ili kufukia malengo yaliokusudiwa.

Comments