Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli jana Jumapili ameungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitali.
Akiwa mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walisali ibada ya asubuhi katika kanisa hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.
Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo walielezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na walimuombea afya njema.
“Nimejisikia furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia” alisema Mama Mabula.


chanzo;mpekuziblog.
Comments