Askari
wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kuzuia tukio la ujambazi
katika mapambano ya kurushiana risasi na watu waliosadikiwa kuwa ni
majambazi na kuua wawili kati yao.
Taarifa
iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari
imesema kuwa mnamo tarehe 19.12.2016 majira ya saa 1:45 jioni katika
Kijiji cha Busisya, Wilaya ya Rungwe, Askari Polisi walipata taarifa za
siri za kuwepo kwa majambazi wenye silaha ambao walikuwa na lengo la
kufanya uvamizi katika Duka la Mfanyabiashara wa soda na bia za jumla
ambaye pia ni wakala wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao.
Askari
hao walianza kuwafuatilia majambazi hao na muda wa saa 1:45 jioni
askari walikutana na majambazi hao wakiwa wamepakiana katika pikipiki
ambapo baada ya majambazi hao kugundua kuwa wanafuatiliwa na askari
walianza kuwarushia risasi askari na ndipo yalitokea majibizano ya
risasi kati ya askari na majambazi hao.
Askari
walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili ambao walifariki papo
hapo na mmoja wao aliweza kutupa silaha aliyokuwa akiitumia na kukimbia.
Aidha
katika tukio hilo silaha bunduki tatu pamoja na risasi tisa ziliweza
kupatikana zilizokuwa zinatumiwa na majambazi hayo. Silaha hizo ni Mark
IV yenye namba 38482 na risasi mbili, Short Gun Greener yenye namba
G.73878 na risasi 01 na Gobole lililotengenezwa kienyeji ambalo halina
namba na risasi 06.

chanzo;mpekuziblog.
Comments