Kikwete amtembelea Rais wa Namibia.

Rais Mstaafu wa Tanzania na Kamishna wa Kamisheni ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu Duniani (Education Commission on Financing Global Education Opportunity), Jakaya Kikwete jana alikutana na Rais wa Namibia, Hage Geingob alipomtembelea mapumzikoni huko Swakopmund, Namibia.

Katika nafasi yake ya Mjumbe Maalum wa Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu amemkabidhi Rais Hage Geingob Ripoti ya Kamisheni hiyo yenye mapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu (A Learning Generation).

Mpango huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja (miaka 30). Azma kuu ya Mpango huo ni kuwezesha ifikapo mwaka 2040, watoto wote kote duniani wawe wanapata elimu iliyo sawa, na kwa kiwango cha ubora unaolingana dunia nzima.

CHANZO: zanzibar24.

Comments