Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza
Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa
wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga katika Jiji la
Mwanza pamoja na mikoa mingine mpaka hapo mamlaka husika
zitakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa
kuwashirikisha wamachinga wenyewe.
Rais
Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo
hilo tarehe 06 Desemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya
kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie
ngazi.
chanzo;mpekuziblog.
Comments