DPP Zanzibar: Hatutamvumilia mwendesha mashtaka yeyote atakayejihusisha na Rushwa.

Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP) Ibrahimu Mzee amesema afisi yake haitamvumilia muendesha mashtaka au wakili yeyote atakaetuhumiwa kuhusika na rushwa kwa lengo la kunyima haki au kupindisha sheria .

DPP aliyasema hayo ukingoni mwa mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya haki jinai uliowashirikisha watendaji wa vyombo vya sheria wakiwemo polisi ,mawakili na waendesha mashtaka wakati akifunga mkutano huo.

Amesema kwa muda mrefu dhana ya rushwa na malalamiko ya wananchi yamekuwa yakielekezwa kwa watendaji hao hivyo sio busara kukaa kimya na kufumbia macho suala hilo kwani linaivunjia heshima taasisi hiyo.

Dpp huyo amesisitiza kwa taassisi nyengine kusimamia mambo matatu ili kumaliza vitendo vya udhalilishaji na kesi za jinai nchini aliyoyataja kuwa ni uwajibikaji, ushirikiano wa kitaasisi katika kufanya kazi na kuepuka rushwa kwa watendaji.

chanzo:zanzibar24.

Comments