Wakati akielekea kuumaliza mwaka mmoja tangu aingie madarakani,
amesema amekuwa akitumia juhudi zake binafsi pasipo kusubiri ruzuku
kutoka serikalini kutekeleza ahadi zake.
Kumbilamoto ameyazungumza hayo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii, ambapo amesema yeye kama
Diwani aliona ni vema atumie juhudi zake akishirikiana na wadau kutoka
katika kata yake kutekeleza jukumu lake kwani akisubiri ruzuku
angechelewa.
Ameeleza badhi ya mafanikio kwa upande wa sekta ya afya
aliyoyawezesha katika kata yake kuwa ni, kupunguza kilio cha kina mama
kwa kupeleka vitanda vya kujifungulia katika Zahanati ya vingunguti.
Ili kuepukana na tatizo la giza katika Zahanati hiyo, amepeleka
genereta moja, feni nne, na televisheni moja kwa ajili ya kupata habari
mbalimbali.
Kumbilamoto pia amesema amefanikisha ununuzi wa magari mawili ya
kubebea wagojwa kitu ambacho kilikua kero ya muda mrefu na kupelekea
baadhi ya wagojwa kupoteza maisha kwa ukosefu wa usafiri.
Katika kuhakikisha suala la usafi katika wodi ya wazazi, amewajengea
choo cha ndani katika wodi hiyo pamoja na mashine moja ya kufulia nguo
za wagojwa.
Pia, amesema ndani ya mwaka huu amepeleka mashine ya kupimia presha,
kisukari pamoja na tochi ya kupimia ugonjwa wa tons (mafindofindo)
mapanzia ya kufunikia wagojwa wakizidiwa ama kufariki.
Aidha, amesema amefanikisha upanuzi wa maabara ya Zahanati hiyo.
“Kwa upande wa sekta ya afya hayo ndio mazuri na makubwa
niliyoyafanya na kama ambavyo niliahidi kwa wananchi wangu kwamba
nikiingia nitatatua kero zote za upande wa afya,” amesema Kumbilamoto.
Hata hivyo, anasema kwa upande wa elimu ukiacha misaada kutoka
serikalini, aliyoyafanya yeye makubwa, ni kupeleka mashine moja ya
kuzalishia nyaraka (printer) katika shule ya sekondari vingunguti ikiwa
pamoja na kulipa deni la umeme 500,000 ambalo lilipelekea shule hiyo
kukosa umeme mwaka mzima.
Bila kusahau ahadi zake kwa vijana Diwani huyo ametekeleza moja ya
ahadi zake kwa kuwapatia jezi seti 14 katika vikundi vya timu za mpira
na vikundi vya mazoezi ya asubuhi (joging clubs) katika kata yake.
Katika utekelezaji wa shughuli za kijamii Diwani Kumbilamoto amesema,
amefanikiwa kufufua vyoo viwili vya umma ambavyo vipo nje ya machinjio
na relini.
“Haya ni nusu na robo kati ya mambo ambayo niliahidi binafsi
kuyatekeleza, kwa mwaka huu nimeyafanya hayo, naamini miaka ijayo
nitafanya zaidi ya haya kwa ushirikiano wa wananchi wangu,” amesema.
chanzo; zanzibar24.
Comments