POLISI mkoani Singida inamshikilia dereva wa gari dogo la abiria la Super Mamuu, kwa tuhuma za kuendesha kwa mwendo wa hatari.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Mayala Towo, alimtaja dereva
anayeshikiliwa kuwa ni Saidi Juma (26) mkazi wa Dodoma ambaye inadaiwa
siku ya tukio alikuwa anaendesha basi aina ya Nissan Civilian lenye
namba za usajili T.360 DAY huku akicheza muziki.
Inaelezwa
kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 4, mwaka huu, saa 11: 00 jioni katika
Mji Mdogo wa Itigi wilayani Manyoni wakati mtuhumiwa akiwa na wenzake
watatu, alipoendesha gari hilo kwa mwendo wa hatari kwa kucheza muziki
huku akiachiana usukani na wenzake hao wakati gari hilo likiwa kwenye
mwendo.
Kamanda
Towo aliwataja watuhumiwa wengine ambapo pia wanashikiliwa na Polisi
kuwa ni Joseph Ramadhan (27), Ezekiel Joseph (24) na Sebastian Godfrey
(23) wote wakazi wa Majengo, Itigi.
chanzo;mpekuziblog.
Comments